Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Monday, 13 April 2015

Transfoma yaripuka Chuo Kikuu Nairobi, mmoja afa

Mwanafunzi mmoja wa Mkenya ameaga dunia na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa wakati wakikimbia, baada ya transfoma ya umeme kuripuka katika bweni moja la wanachuo katika Chuo Kikuu cha Nairobi kabla ya alfajiri ya leo. Mripuko huo uliibua wasiwasi na wahaka katika mabweni ya wanachuo wakidhani kuwa wamevamiwa. Katika tuki hilo lililotokea mapema leo, baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi waliruka madirishani ili kujinusuru, ikiwa zimepita siku chache tu baada ya wanamgambo wa kundi la kigaidi la al Shabab kukishambulia Chuo Kikuu cha Garissa na kuuwa wanafunzi zaidi ya 100. Peter Mbithi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi amesema kuwa, mwanafunzi aliyefariki dunia alikuwa kati ya wale walioruka kutoka kwenye bweni lao lililoko katika ghorofa tano, wakihofia majengo ya chuo hicho yamevamiwa. Walioshuhudia mripuko huo wa transfoma ya umeme wamesema kuwa iliripuka saa 10.30 alfajiri ya leo kwa saa za Kenya na hivyo kusababisha wanafunzi wa kike kuanza kupiga kelele na hofu hiyo kuenea pia kwa upande wa wavulana, na kisha wanafunzi wakaamka na kuanza kujaribu kutoka nje

No comments:

Post a Comment