Kamisheni Kuu ya Uchaguzi nchini Sudan imetangaza kuwa Rais wa
sasa wa nchi hiyo Omar al Bashir ameshinda tena kiti cha rais kwa kupata
asilimia 94 ya kura za uchaguzi uliofanyika mwezi huu.
Taarifa ya
kamisheni hiyo pia imesema chama tawala cha Congresi ya Taifa kimeshinda
uchaguzi wa Bunge kwa kupata viti 323 kati ya viti vyote 426. Mkuu wa
Kamisheni ya Uchaguzi ya Sudan, Mokhtar al-Assam amesema asilimia 46.4
ya watu karibu milioni 13 waliojiandikisha ilishiriki katika zoezi hilo
lililofanyika kwa siku nne kuanzia Aprili 13.
Al Bashir mwenye umri
wa miaka 71 amepata kura milioni 5 lakini mbili elfu 52 na 478 kati ya
kura zote sahihi milioni 5, 584 elfu na 863. Mpinzani wake wa karibu
katika uchaguzi huo, Fadhl Assayyid Shuaib amepata asilimia 1.43 ya
kura.
Al Bashir ambaye ameiongoza Sudan kwa kipindi cha miaka 25
anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa tuhuma za kutenda
jinai za kivita katika jimbo la Darfur.
No comments:
Post a Comment