Mashambulizi yanayolenga raia wa kigeni yamewalazimisha wahajiri
zaidi ya elfu moja kukimbia nyumba zao katika mji wa Durban nchini
Afrika Kusini.
Msemaji wa polisi ya mji huo, Thulani Zwane amesema kuwa wahajiri hao wametishwa na wenyeji wakitakiwa kuondoka katika nyumba zao na wamekimbilia vituo vya polisi kwa kuhofia maisha yao.
Machafuko hayo yameshadidi zaidi tangu Jumatatu iliyopita huku wahajiri zaidi wakiendelea kukimbia nyumba zao baada ya kutishiwa na wenyeji. Hata hivyo hakuna kesi yoyote ya mauaji iliyoripotiwa hadi hivi sasa.
Jumatano iliyopita askari usalama walitumia mipira ya maji na gesi za kutoa machozi kutawanya waandamanaji wa kigeni wengi wao wakiwa Waafrika, waliokuwa wakipinga machafuko na mashambulizi yanayowalenga nchini Afrika Kusini.
Mwaka 2008 machafuko kama haya yanayolenga raia wa kigeni nchini Afrika Kusini yalisababisah vifo vya watu 62.

No comments:
Post a Comment