
Polisi nchini Italia wanasema kuwa wamewakamata watu 18 wanaoshukiwa
kuwa wanachama wa Islamic State kutoka nchini Afghanistan na Pakistan
katika oparesheni kubwa ya kupambana na ugaidi.
Wanasema kuwa
wawili kati ya washukiwa hao wanaaminiwa kuwa walinzi wa aliyekuwa
kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden na wengine wanashukiwa kuhusika
kwenye mashambulizi nchini Pakistan likiwemo shambulizi lililotokea
kwenye soko la Peshawar.
Oparesheni hiyo ilikuwa imeendeshwa kwenye kisiwa cha Italia cha Sardina .
Polisi
walisema kuwa kundi linalofanyiwa uchunguzi lilikuwa limewapangia
wanachama wake kuingia nchini Italia wakiwa na vyeti vya kufanya kazi au
kama watafuta hifadhi.
No comments:
Post a Comment