Naibu Katibu Mkuu wa harakati ya
muqawama wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema Saudi Arabia
itashindwa tu katika uvamizi wake dhidi ya Yemen. Sheikh Naeem Qasim,
ameongeza kuwa dunia leo inashuhudia kipigo cha kufedhehesha inachopata
Saudi Arabia; na licha ya mashinikizo yote, harakati ya wananchi ya
Ansarullah pamoja na jeshi la Yemen zinaendelea kudhibiti maeneo mengi
ya kaskazini na kusini mwa nchi hiyo. Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah
amesisitiza kuwa kadiri vita vikichukua muda mrefu zaidi ndivyo
kushindwa kwa Saudia kutavyozidi kudhihirika. Katika upande mwengine
ripoti kutoka Yemen zinaeleza kuwa majeruhi walioko kwenye mkoa wa
Sa’dah wako katika hali mbaya kutokana na kuzingirwa mkoa huo na
kushindwa misaada ya tiba kuwafikia watu hao. Muhammad Hajr, Mkurugenzi
Mkuu wa hospitali ya al Jamhuri mkoani Sa’dah amesema kuendelea
mashambulio ya ndege za kivita za Saudi Arabia na kushindwa kufika
misaada ya tiba kutokana na mzingiro kumezifanya hali za majeruhi katika
mkoa huo ziwe mbaya zaidi. Akiashiria kuendelea mashambulio ya ndege za
kivita za utawala wa Aal Saud dhidi ya taasisi muhimu na miundomsingi
ya Yemen, Muhammad Hajr ameziomba jumuiya za kimataifa kufanya jitihada
ili kuepusha kutokea maafa ya kibinadamu nchini humo. Wito huo umetolewa
katika hali ambayo kwa mara nyengine tena ndege za kivita za Saudia
jana zilizuia kuingia kwenye anga ya Yemen na kutua kwenye uwanja wa
ndege wa Sana’a ndege ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyobeba misaada
ya kibinadamu na shehena za madawa na vyakula.
Katika medani za mapambano, ripoti
zinaeleza kuwa mkoa wa Ma’rib unadhibitiwa kikamilifu na harakati ya
Ansarullah. Duru moja ya kijeshi ya Yemen imetangaza kuwa baada ya
vikosi vya gadi ya Rais vyenye mfungamano na Rais wa zamani wa nchi hiyo
Ali Abdullah Saleh kujiunga na harakati ya wananchi ya Ansarullah, mkoa
wa Ma’rib ulioko katikati mwa nchi hiyo uko chini ya udhibiti kamili wa
harakati hiyo ya wananchi…
No comments:
Post a Comment