Kiongozi mmoja wa zamani wa mahakama
nchini Uingereza amesema kuwa, vijana wengi wa nchi hiyo wamejiunga na
kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh baada ya kurubuniwa. Nadhir
Afdhal, mmoja wa viongozi wa Kiislamu aliyewahi kuhudumu katika vyombo
vya mahakama nchini Uingereza amesema kuwa, mfumo wa kuwarubuni vijana
unaotumiwa hii leo ndio chanzo cha vijana kuendelea kujiunga na magaidi.
Amesisitiza kuwa, Uingereza na nchi nyingine za dunia zinatakiwa
kuchukua hatua za kisasa katika kukabiliana na mfumo huo hatari
unaowaingiza vijana wengine katika wimbi la ugaidi.
Kwa mujibu wa msomi huyo, magaidi
wanatumia njia za kisasa katika kujitangaza, suala ambalo limewafanya
vijana wengi waathiriwe na propaganda hizo. Hayo yamekuja wakati ambao
hivi karibuni, ilitangazwa habari ya kutiwa mbaroni mtoto wa
mwanaharakati mmoja wa chama cha Leba nchini Uingereza akiwa pamoja na
Waingereza kadhaa waliokamatwa katika mpaka wa Uturuki wakielekea Syria
kwa ajili ya kujiunga na makundi ya kigaidi yanayopigana na jeshi la
serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment