Monday, 27 April 2015
Wanne wauawa katika mashambulio ya Israel Golan
Watu wanne wameuawa katika mashambulio ya anga ya utawala wa
Kizayuni wa Israel kwenye miinuko ya Golan inayokaliwa kwa mabavu na
utawala huo, karibu na mpaka wa Syria. Wahanga wa mashambulio hayo ya
Israel ya jana usiku yaliyotekelezwa karibu na mji wa Majdal Shas, bado
hawajatambuliwa hadi sasa. Israel imefanya shambulio hilo jana usiku
kwenye miinuko ya Golan, siku mbili baada ya utawala huo kuzishambulia
kambi za jeshi la Syria huko katika eneo Qalamoun karibu na mpaka wa
nchi hiyo na Lebanon. Miinuko ya Golan imekuwa ikikaliwa kwa mabavu na
utawala wa Kizayuni wa Israel tangu muongo wa 60. Utawala wa Tel Aviv
uliikalia kwa mabavu ardhi ya miinuko ya Golan yenye ukubwa wa kilomita
1200 wakati wa Vita vya Siku Sita mnamo mwaka 1967na kisha kulitwaa eneo
hilo mwaka 1981
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment