Sunday, 26 April 2015
AI yataka kupanuliwa oparesheni za kuokoa wahajiri
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limetaka
kupanuliwa oparesheni za kuwatafuta na kuwaokoa wahajiri wanaolekea
barani Ulaya kutokana na kusafiri katika mazingira hatari katika bahari
ya Mediterranean. Gauri van Gulik, Naibu Meneja wa shirika hilo la haki
za binadamu barani Ulaya amesema kuwa operesheni za uokoaji zinapaswa
kupanuliwa hadi kwenye maeneo ya karibu na pwani za Libya. Amesema
wahajiri mara kwa mara wamekuwa wakitumia boti kuukuu ili kujaribu
kufikia pwani za nchi za Ulaya na kwamba polisi wa doria wamekuwa
wakikagua maeneo ya karibu na mipaka ya Italia pekee. Naibu Meneja wa
Amnesty International barani Ulaya amesema hayo kufuatia ajali ya boti
ya hivi karibuni katika bahari ya Mediterranean iliyouwa watu 800.
Tarehe 16 mwezi huu msemaji wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja
wa Mataifa (UNHCR) alithibitisha kuwa watu 800 walikufa maji kufuatia
ajali ya boti katika bahari hiyo. Boti hiyo ilizama katika umbali wa
kilomita 96 kutoka pwani ya Libya wakati ilipokuwa inaelekea Italia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment