Viongozi wa Syria wamesema kuwa wako tayari kutuma vikosi vya ulinzi
katika kambi ya wakimbizi ya Yarmuk huko kusini mwa Damascus mji mkuu wa
nchi hiyo. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema kuwa nchi hiyo
iko tayari kutuma vikosi maalumu vya ulinzi katika kambi ya wakimbizi
ya Yarmuk ili kuikomboa kambi hiyo kutoka kwa wanamgambo wa Daesh.
Fadhil Miqdad ameyasema hayo katika mazunumzo kati yake na Mjumbe wa
Harakati ya Ukombozi wa Palestina(PLO).
Miqdad ameongeza kuwa taasisi za kimataifa pia zinapasa kuchukua hatua kali na za kivitendo ili kuzuia jinai za kundi la Daesh katika kambi ya Yarmuk na kutafuta njia za kutatua matatizo ya wakimbizi wa Kipalestina waishio katika kambi hiyo. Kituo cha Haki za Binadamu cha Syria kimeripoti kuwa, raia wasiopungua 13 wameuawa katika kambi hiyo siku sita zilizopita na wakazi elfu ishirini wa kambi ihiyo pia wanakabiliwa na uhaba wa maji na chakula.

No comments:
Post a Comment