Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya
Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuongezwa muda wa
kushikiliwa korokoroni Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa Harakati ya
Kiislamu ya al-Wifaq ya Bahrain hakusaidii chochote katika kuyapatia
ufumbuzi matatizo ya nchi hiyo. Marzieh Afkham amebainisha kwamba,
kuendelea kutawala mazingira ya kipolisi nchini Bahrain kunaifanya hali
ya mambo nchini humo izidi kuwa tata. Afkham amesisitiza kuwa, watawala
wa Bahrain wanapaswa kuzingatia suala la mazungumzo na kuheshimu matakwa
ya wananchi sambamba na serikali ya Manama kuchukua hatua zitakazoandaa
mazingira ya kuweko hali ya kuaminiana. Msemaji wa Wizara ya Mashauri
ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema bayana kwamba,
kuheshimu matakwa ya wananchi ni jambo muhimu mno. Wakati huo huo,
mwanazuoni mashuhuri nchini Bahrain Sheikh Issa Qassim amesema kuwa,
kuendelea kutiwa mbaroni wanaharakati wa kisiasa ni ishara ya wazi
kwamba, watawala wa Manama wameng’ang’ania kuendeleza siasa za
ukandamizaji.
No comments:
Post a Comment