Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Tuesday, 21 April 2015

Wasiwasi wa viongozi wa Rwanda kuhusiana na wimbi la wakimbizi wa Burundi

Viongozi wa Rwanda wameelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusiana na kuongezeka wimbi la wakimbizi wa Burundi nchini humo. Wizara ya Udhibiti wa Migogoro na Masuala ya Wakimbizi ya Rwanda imesema kuwa kufikia sasa idadi ya wakimbizi wa Burundi walioingia nchini humo imepindukia 6570. Wakimbizi wengi wamekimbilia Rwanda na nchi nyinginezo jirani kutokana na hofu ya kuongezeka ghasia nchini kwao katika kipindi hiki cha kukaribia kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo, uchaguzi ambao umepangwa kufanyika tarehe 26 mwezi Juni. Wanadiplomasia wanasema wakimbizi wengi wa Burundi wanakimbilia Rwanda kutokana na nafasi yake nzuri ya kijiografia katika eneo la Afrika ya Kati.
Uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi wa kuwania kiti cha rais kwa mara ya tatu mfululizo umezua hofu na wasiwasi mkubwa nchini humo. Viongozi wa muungano wa vyama vitano vya upinzani wa The Alliance for Democratic Change (ADC), hadi sasa hawajaafikiana kuhusiana na mgombea wa pamoja katika uchaguzi mkuu huo. Wanasema wanataka kumchagua mgombea anayefaa ambaye bila shaka atamshinda Pirre Nkurunziza katika uchaguzi huo. Wakati huohuo, ghasia ambazo zimekuwa zikifanywa na wanamgambo wa tawi la vijana wa chama tawala zimezidisha wasiwasi na hofu nchini humo na hivyo kufanya maelfu ya wakimbizi kutafuta usalama nje ya mipaka ya nchi yao. Wanamgambo hao wanaojulikana kwa jina la Imbonerakure waliwauwa kwa umati watu 47 huko kaskazini mwa Buundi katika kipindi cha kati ya tarehe 30 Disemba 2014 hadi tarehe 3 Januari mwaka huu. Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kuwa mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Cibitoke yalitekelezwa na vijana hao kwa ushirikiano wa askari usalama wa nchi hiyo.
Katika upande wa pili Saber Azam, mwakilishi wa shirika linalohudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR huko Rwanda amesema kuwa wakimbizi wa Burundi wasiopungua 800 huingia nchini humo kila siku ambapo wengi wao ni wanawake na watoto. Shirika hilo la kimataifa limeimarisha shughuli zake huko katika eneo la Pembe ya Afrika na Ukanda wa Maziwa Makuu tokea mwaka 2012, ambapo linawadhaminia wakimbizi mahitaji na suhula za afya, chakula na masomo. Ripoti zinasema kuwa mbali na wakimbizi wa Burundi kuelekea Rwanda pia wamekuwa wakikimbilia nchi jirani za Tanzania, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa mujibu wa mipango ya UNHCR, tokea mwaka 2012 hadi 2017 shirika hilo linatazamia kuwapa wakimbizi wa Burundi wapatao elfu 50, makazi ya kudumu

No comments:

Post a Comment