Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, kundi la kigaidi la
Daesh lilianzishwa mwaka 2006 kwa usimamizi wa Wamarekani. Rais wa Syria
amesisitiza kwamba, kundi hilo la kigaidi lilianzishwa na Marekani na
kuongeza kuwa, muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kwa ajili
ya kupambana na kundi hilo la kigaidi hadi sasa haujawa na nia ya dhati
ya kuwatokomeza magaidi hao. Rais Assad ameikosoa Ufaransa na baadhi ya
madola mengine ya magharibi kwa kuwaunga mkono wapinzani wa Syria na
kusema bayana kwamba, kundi la kigaidi la Daesh lilianzishwa mwaka 2006
huko Iraq kwa usimamizi na uongozi wa Marekani. Aidha Rais Assad
amekanusha vikali madai kwamba, jeshi la Syria limetumia mabomu ya
kemikali katika mashambulio yake huko Idlib na kubainisha kwamba,
Damascus haioni haja ya kufanya hivyo. Kuhusiana na ushirikiano wa Syria
na Magharibi, Rais Bashar al-Assad amesema kuwa, endapo Wamagharibi
wataiahidi na kuihakikishia Syria kwamba, wataacha kuwaunga mkono
magaidi, basi serikali ya Damascus iko tayari kushirikiano nao
No comments:
Post a Comment