Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 29 April 2015

Iran: Mashambulizi ya Saudia, Yemen yasitishwe

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametaka kusimamishwa haraka mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya raia wa Yemen. Marzieh Afkham amesema anataraji kuwa Ismail Sheikh Ould Ahmad, mjumbe mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen atachukua hatua za maana ili kusitisha mashambulizi ya kijeshi ya Saudi Arabia dhidi ya watu wasio na hatia wa Yemen. Bi Afkham ameongeza kuwa kuna udharura wa kuzuia hali ya mambo ya Yemen isiwe mbaya zaidi, kama hatua muhimu ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.
Kuhusu kuanza kazi mjumbe mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inataraji kuwa Ismail Sheikh Ould Ahmad atachukua hatua za maana ili kusimamisha mashambulizi ya kijeshi ya Saudi Arabia na kuanza haraka mazungumzo kati ya makundi na vyama vyote vya nchi hiyo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa mashambulizi ya kijeshi ya Saudia huko Yemen  ni kosa kubwa na mahesabu mabaya na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuwa mgogoro wa Yemen unapaswa kupatiwa ufumbuzi kwa njia za kisiasa na kwa kufanyika mazungumzo ya makundi yote ya Wayemeni ili kuasisi serikali ya umoja wa kitaifa.

No comments:

Post a Comment