Maelfu ya wakazi wa mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, waliandamana jana kuunga mkono sheria mpya za uchaguzi.
Waandamanaji hao walipiga nara zinazounga mkono sheria mpya za
uchaguzi zilizopasishwa na Bunge tarehe 7 mwezi huu wa Aprili. Sheria
hizo mpya zinawazuia wanachama wa serikali iliyoondoka madarakani
kushiriki katika uchaguzi ujao.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burkina Faso, Auguste Denise Barry
amesema kuwa serikali ya mpito ya nchi hiyo ina azma ya kukamilisha
kipindi cha mpito kwa mafanikio.
Kwa mujibu wa sheria mpya za uchaguzi za Burkina Faso, mbali na kambi
ya rais wa zamani wa nchi hiyo Blaise Compaoré, vyama vyote ambavyo
viliunga mkono mpango wa kiongozi huyo wa kubadili katiba ili kumruhusu
agombee tena kiti cha rais kwa zaidi ya mara mbili, vitazuiwa kushiriki
katika uchaguzi ujao. Blaise Compaoré alilazimika kung'atuka madarakani
Oktoba mwaka jana baada ya kushadidi wimbi la maandamano ya wananchi
waliokuwa wakipinga utawala wake
No comments:
Post a Comment