Kikosi cha askari wa kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika
eneo la Darfur huko magharibi mwa Sudan (UNAMID) kimekanusha madai
yaliyotolewa na serikali ya Khartoum dhidi ya askari wa kikosi hicho.
UNAMID imekanusha madai kwamba askari wake waliua raia katika mji wa
Kaas huko kusini mwa Darfur na kusisitiza kuwa kikosi hicho kilijibu
mashambulizi katika hali ya kujihami.
Afisa mwandamizi wa UNAMID amesema si sahihi kuwatuhumu askari wa
kikosi cha kimataifa kwamba wameua raia na kwamba lengo la kutolewa
tuhuma kama hizo ni kupotosha fikra za waliowengi nchini Sudan.
Jana Jumamosi Gavana wa jimbo la Darfur ya Kusini nchini Sudan
aliwatuhumu askari wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika na
Umoja wa Mataifa katika eneo la Darfur UNAMID kuwa wameua raia saba
wasio na hatia katika jimbo hilo. Gavana Adam Jarunnabiy alisema
kumeundwa tume maalumu ya kuchunguza mauaji ya raia hao
No comments:
Post a Comment