Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Sunday, 26 April 2015

Wawili wauawa kwa risasi za polisi Bujumbura Burundi

Raia wawili wa Burundi wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika machafuko yaliyotokea leo huko Bujumbura mji mkuu wa Burundi. Machafuko hayo ya leo yametokea katika maeneo mengi ya mji mkuu Bujumbura, wakati watu walipoandama kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo ya kuamua kugombea urais kwa muhula mwingine wa tatu. Watu walioshuhudia wameongeza kuwa mmoja wa waandamanaji katika machafuko ya leo huko Bujumbura ameuawa katika wilaya ya Ngagara na mwingine katika wilaya ya Musaga huko huko Bujumbura. Habari zinasema kuwa polisi wa Burundi walitumia silaha za moto, gesi ya kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya waandamanaji. Leonce Ngendakumana Kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Frodebu amesema kuwa, wameitisha maandamano ya amani, hata hivyo polisi na wanamgambo wa chama tawala cha Burundi wamewafyatulia risasi hai waandamanaji

No comments:

Post a Comment