Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 8 April 2015

MSF: Hali ya Aden, Yemen inazidi kuwa mbaya
















Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka imetahadharisha juu ya kuzidi kuwa mbaya hali ya mambo ya mji wa Aden huko kusini mwa Yemen, huku Saudi Arabia ikishadidisha mashambulilzi yake ya anga dhidi ya nchi hiyo ya Kiarabu. Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka(MSF) imetoa tahadhari hiyo Jumanne hii ikisema kuwa hali ya mambo katika mji wa Aden inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku. Mji wa Aden umegeuka na medani ya mapigano makali kati ya vikosi vitiifu kwa Rais wa Yemen aliyejiuzuluAbdurabbuh Mansour Hadi  na wanachama wa makundi ya wananchi wanaoungwa mkono na wapiganaji wa Kihouthi. Watu wanaoshuhudia mapigano hayo wamesema kuwa vikosi vya majini vya Saudia vimeyashambulia maeneo ya wanamapinduzi katika mji wa Aden, suala lililokanushwa na Saudi Arabia.

No comments:

Post a Comment