Ndege za kivita za Saudi Arabia jana usiku kwa mara nyingine tena
zimeyashambulia maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Yemen Sana'a. Ndege za
kivita za Saudi Arabia jana usiku zililishambulia kwa mara kadhaa eneo
la al al-Urqub Khulan huko katika mji mkuu Sana'a. Saudi Arabia wiki
iliyopita ilitangaza kuwa imesitisha mashambulizi yake ya siku 27 huko
Yemen baada ya kuuwa raia wasio na hatia wa Yemen zaidi ya elfu tatu
wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kubomoa miundo mbinu ya nchi hiyo,
hata hivyo masaa mawili baada ya kutangaza kusitisha hujuma zake za
kijeshi katika nchi hiyo ya Kiarabu, ndege za utawala huo vamizi kwa
mara nyingine tena zilianza kuyashambulia maeneo ya raia na kubomoa
miundo mbinu ya Yemen.
Wakati huo huo habari kutoka Yemen zinarifu kuwa, makundi ya
wanamapinduzi wa nchi hiyo wamewataka wananchi kufanya maandamano
makubwa ya mshikamano hii leo kote nchini humo, ili kumpinga adui Saudi
Arabia.
No comments:
Post a Comment