Maafisa wa Afrika Kusini wamemtia mbaroni binti mwenye umri wa miaka 15
aliyekuwa amepanga kuondoka nchini humo kwa lengo la kujiunga na kundi
la wanamgambo wa kitakfiri la Daesh huko Syria. Binti huyo ambaye jina
lake halikufahamika alinaswa Jumapili wiki hii katika uwanja wa ndege wa
mjini Cape Town. Binti huyo alikutwa katika ndege ya shrike la ndege la
Uingereza akiwa ameketi ndani ya katika sehemu inayojulikana kama
"business class" kwa ajili ya kuelekea katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Oriver Tambo huko Johannesburg. Binti huyo mweney umri wa
miaka 15 alipanga kuelekea Uturuki kwa kutumia usafiri wa ndege, na
kisha kusafiri kwa kutumia baraka ili kuelekea Syria kwa minajili ya
kujiunga na Daesh. Ndugu na wazazi wa mtoto huo wamesema kuwa mwezi
uliopita binti wao ajiingiza sana katika masuala ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment