Mrengo wa upinzani nchini Burundi unaoundwa na vyama tisa,
umemtangaza Jean de Dieu Mutabazi kuwa ndiye atayapeperusha bendera yao
katika uchaguzi ujao wa rais nchini humo. Muungano huo unaojulikana kwa
jina la Participatory Opposition Coalition in Burundi COPA kwa kifupi
umetangaza kuwa, umemteua Jean Mutabazi kuwa mgombea wake katika
uchaguzi ujao wa Rais nchini Burundi uliopangwa kufanyika Juni mwaka
huu. Jean Mutabazi ambaye pia ndiye mwenyekiti wa muungano huo wa COPA
amesema kuwa, muungano huo wa vyama vya upinzani haumuhofii mgombea
yeyote yule akiwemo wa chama tawala CNDD-FDD Rais Pierre Nkurunziza.
Muungano wa COPA uliundwa Septemba mwaka jana na umejindaa kushiriki
vizuri katika uchaguzi mkuu ujao nchini Burundi. Wiki iliyopita pia
chama cha The National Rally for Change RANAC kwa kifupi kilimtangaza
Rais wa zamani wa nchi hiyo Domitien Ndayizeye kuwa mgombea wake katika
uchaguzi ujao wa Rais nchini Burundi. Aidha chama cha FRODEBU kwa upande
wake nacho kimemteua Dr Jean Minani kuwa mgombea wake wa kiti cha urais
katika uchaguzi ujao
No comments:
Post a Comment