Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Friday, 10 April 2015

Kiongozi Muadhamu atoa msamaha kwa wafungwa

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei ametoa msamaha na punguzo la adhabu kwa iddai kadhaa ya wafungwa wanawake kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Bibi Fatma Zahra (as) binti Mtukufu wa Mtume Muhammad (saw). Kiongozi Muadhamu ametoa msamaha na punguzo hilo la adhabu baada ya kuafiki ombi la Ayatullah Sadiq Amoili Larijani Mkuu wa Vyombo vya Mahakama hapa nchini aliyewasilishwa kwake akitaka kusamehewa na kupunguziwa adhabu idadi kadhaa ya wafungwa wanawake waliotimiza masharti ya kupatiwa msamaha au punguzo hilo. Ikumbukwe kuwa, Waislamu hususan wa madhehebu ya Shia katika maeneo mbalimbali duniani tangu jana usiku walianza kuadhimisha tukio la kuzaliwa binti wa Mtume wetu Muhammad (saw), Bibi Fatimatu Zahra (as) linalosadifiana na siku ya leo ya tarehe 20 Mfunguo Tisa Jamadithani. Sherehe hizo zinafika kileleni leo kwa kufanyika vikao vya mihadhara na majlisi za sherehe zinazotumbuizwa kwa tungo za kumsifu Mtume (saw), binti yake mtukufu na Ahlibaiti zake watoharifu. Siku ya kukumbuka kuzaliwa mwanamke bora kuliko wote duniani, yaani Fatima binti Muhammad (saw) hapa nchini Iran inasherehekewa kama Siku ya Mama, ambapo akina mama huenziwa na kutunzwa.

No comments:

Post a Comment