Ndege za kivita za Saudi
Arabia zimeendeleza mashambulizi yake ya kichokozi katika maeneo tofauti
ya Yemen ikiwemo miji ya Hajja na Taiz na maeneo mengine ya nchi hiyo.
Aidha ndege za kivita za utawala wa Aal Saudi zimetekeleza mashambulizi
makali dhidi ya mji wa al-Dhahir uliopo katika mkoa wa Saada na
kupelekea watu wengi kuuawa na kujeruhiwa. Hii ni katika hali ambayo,
wanamapambano wa Yemen kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo
wamefanikiwa kudhibiti kambi ya jeshi ya kikosi cha 35 iliyokuwa
ikidhibitiwa na magaidi wa al Qaeda katika mkoa wa Taiz ambapo
wamefanikiwa pia kuwafurusha matakfiri hao kutoka eneo hilo. Aidha
wanamapambano wa Yemen wamedhibiti ngome muhimu za magaidi wa kitakfiri
katika mji wa Marib na eneo la al-Wahat katika mkoa wa Hajja. Kwa mujibu
wa duru za habari, ndege za Saudia na waitifaki wake zimeshambulia
ngome hizo za magaidi muda mchache tu baada ya kudhibitiwa na
wanamapambano kwa kushirikiana na jeshi la Yemen. Mashuhuda wamenukuliwa
wakisema kuwa, magaidi hao wanaoungwa mkono na Saudia, wamebaki
wakikimbia mitaani huku na kule kufuatia kupokonywa ngome zao walizokuwa
wakizitumia katika kutekeleza mashambulizi na njama dhidi ya taifa hilo
la Kiarabu. Mashambulizi hayo ya ndege za utawala wa Aal Saudi yanajiri
katika hali ambayo siku mbili zilizopita muungano wa nchi
zinazoshirikiana na Riyadh katika hujuma nchini Yemen, zilikuwa
zimetangaza kuhatimisha operesheni hizo
No comments:
Post a Comment