Zeid Ra'ad al Hussein Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja
wa Mataifa amewasili nchini Burundi kwa lengo la kukutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo. Zeid Ra'ad al
Hussein anayefanya safari hiyo ya siku tatu nchini Burundi, atakutana na
kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza na viongozi wengine wa
ngazi za juu wa nchi hiyo. Miongoni mwa ratiba alizopangiwa nchini humo,
ni pamoja na kushiriki kwenye mdahalo unaohusiana na masuala ya haki za
binadamu nchini Burundi na zoezi la uchaguzi wa rais uliopangwa
kufanyika mwezi Juni mwaka huu. Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, hali ya
kisiasa na haki za binadamu nchini Burundi ni ya kusikitisha. Kamishna
Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni raia wa Jordan
alichukua wadhifa huo mwaka jana, na hii ni mara ya kwanza kwa mkuu wa
taasisi hiyo ya kimataifa kushikiliwa na Mwislamu.
No comments:
Post a Comment