Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amezitaka
nchi za Kiislamu zifanye juhudi zaidi za kuutatua mgogoro wa Yemen.
Ali Larijani amesema kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kutekeleza vilivyo majukumu yake kuhusiana na Yemen na zina wajibu wa kufanya juhudi za pamoja za kutatua mgogoro huo.
Dk Larijani amesema hayo katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Spika wa Bunge la Iraq, Salim al Jabouri.
Aidha amesema, kuongezeka mgogoro wa Yemen na kuendelea kuuliwa watu wasio na hatia nchini humo, kuna hasara kwa nchi zote za Kiislamu.
Amesema, inabidi mawasiliano na mashauriano baina ya nchi za Kiislamu yaendelee ili kukomesha maafa hayo ya wananchi wa Yemen.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge la Iraq ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kulipa uzito mkubwa suala la kutatuliwa mgogoro wa Yemen na kuongeza kuwa, Serikali na Bunge la Iraq linaamini kwamba kuna haja ya kuweko mpango maalumu wa hatua kwa hatua wa kutatua mgogoro wa Yemen

No comments:
Post a Comment