Monday, 27 April 2015
HRW: Kesi ya dhidi ya Mursi ilikuwa na dosari
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu(HRW) limekosoa mamlaka
husika za Misri kwa kuendesha kesi isiyo ya kiadilifu na chuki kwa Rais
wa nchi hiyo aliyepinduliwa na jeshi, likisema kuwa upande wa uendeshaji
wa mashtaka uligubikwa na dosari. Taarifa iliyotolewa Jumapili hii na
Human Rights Watch imeeleza kuwa kesi ya Mohamed Morsi iligubikwa na
mchakato wa ukengeukaji wa kanuni, chuki na ukosefu wa ushahidi wenye
kuthibitisha. Taarifa ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu imeongeza
kuwa, upande wa mashtaka ulitegemea sana ushahidi uliotolewa na maafisa
wa kijeshi na polisi na kwamba kesi hiyo dhidi ya Mursi ilichochewa
kisiasa dhidi ya harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri. Sarah Leah
Whitson Mkurugenzi Mkuu wa Human Rights Watch katika eneo la Mashariki
ya Kati na Kaskazini mwa Afrika amesema kuwa Mursi alitajwa kuhusika
katika kesi kwa sababu tu ya uhusiano kati yake na harakati ya Ikhwanul
Muslimin. Bi Whitson amewatuhumu waendesha mashtaka waliomhukumu Mursi
katika kesi ya hivi karibuni kuwa walipuuza vifo vya wafuasi wa Ikhwanul
Muslimin katika ghasia za mwaka 2012 na kutojali kushindwa vikosi vya
usalama kuchukua hatua wakati wa ghasia hizo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment