Serikali ya Morocco imesisitiza upinzani dhidi ya hatua yoyote
ile ya Umoja wa Afrika ya kutaka kusaidia kuipatia ufumbuzi kadhia ya
Sahara Magharibi. Hayo yameelezwa na SalaheddineMezouar, Waziri wa
Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Morocco ambaye amesisitiza kwamba,
nchi yake inapinga kadhia ya Sahara Magharibi kuingiliwa na Umoja wa
Afrika. Salaheddine Mezouar amesema hayo ikiwa ni radiamali kwa matamshi
ya Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika aliyesema katika barua yake kwa
Ban Ki-Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwamba, kuna udharura wa
kuweko himaya ya haki za binadamu ya vikosi vya kusimamia amani katika
eneo la Sahara Magharibi. Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa
Morocco amesema kwamba, barua ya hivi karibuni ya Baraza la Usalama la
Amani la Umoja wa Afrika kuhusiana na kadhia ya Sahara Magharibi
ilionyesha jinsi Umoja wa Afrika unavyoegemea upande mmoja katika kadhia
hiyo. Ni kutokana na sababu hiyo ndiyo maana serikali ya Rabat inapinga
vikali Umoja wa Afrika kuwa na nafasi yoyote ile katika kadhia ya
Sahara Magharibi, amesisitiza waziri huyo wa mashauri ya kigeni wa
Morocco.
No comments:
Post a Comment