Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 29 April 2015

UN: Jamii ya kimataifa imesahau mgogoro wa CAR

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi wake juu ya kusahaulika mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) imesema kuwa, idadi ya wakimbizi laki tisa wa nchi hiyo ambalo ni tatizo mkubwa la kibinaadamu, ni suala ambalo halitakiwi kusahaulika wala kupuuzwa na jamii ya kimataifa. Ripoti hiyo imeeleza kuwa, zaidi ya raia laki nne na 60 elfu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamekimbilia nje ya nchi, huku wengine wapatao laki nne na elfu 36 wakiwa wakimbizi wa ndani. UNHCR imesisitiza kuwa, karibu watu milioni mbili na laki saba wanahitajia msaada wa haraka kutokana na hali yao mbaya. Imeongeza kuwa, licha ya kiwango hicho cha kutia wasiwasi lakini bado asasi husika zimeshindwa kudhamini bajeti kwa ajili ya misaada ya waathirika hao wa mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya kati.
Mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ulishadidi zaidi mnamo mwaka 2013, baada ya kuondolewa madarakani aliyekawa rais wa nchi hiyo, Francois Bozize na waasi wa muungano wa Seleka. Mgogoro ulifuatiwa na mauaji makubwa, ambayo wahanga wake wengi walikuwa Waislamu.

No comments:

Post a Comment