Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Tuesday, 21 April 2015

Kundi la Taliban latangaza vita dhidi ya kundi la Daesh

Gazeti la Khaama Press la Afghanistan limetangaza kuwa, kundi la kitakfiri la Daesh na lile la kigaidi la Taliban yametangaza vita baina yao.
Gazeti hilo limemnukuu mkuu wa polisi wa mkoa wa Helmand, wa kusini mwa Afghanistan akisema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Radio Mashaal, ya Pakistan ambayo ni mwanachama wa kundi la Radio Free Europe.
Nabi Jan Mullahkhil amesema katika mahojiano hayo kuwa, ana ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa makundi hayo mawili ya kigaidi yameingia kwenye vita vikali baina yao.
Mwezi Januari mwaka huu, mkuu wa kundi la Daesh, Abu Bakr al Baghdadi alimtukana mkuu wa kundi la Taliban Mullah Omar akimwita mpuuzi na mbabe mjinga wa kivita ambaye miaka yote 10 iliyopita ameshindwa kuyafikia yaliyofikiwa na Daesh katika kipindi cha miaka miwili.
Februari 21, 2015 pia, wanamgambo wa Daesh walishusha bendera nyeupe ya Taliban katika wilaya ya Charkh huko Afghanistan na kupandisha bendera yao nyeusi. Kuna ushahidi mwingine mbalimbali ambao pia unaonesha kuweko mzozo mkubwa baina ya makundi hayo ya kigaidi.

No comments:

Post a Comment