Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Monday, 20 April 2015

44 wauliwa Yemen katika mashambulizi ya Saudia

Watu wasiopungua 44 wameuliwa nchini Yemen huku hali ya mgogoro ikiendelea kushtadi kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya ndege za kivita za Saudi Arabia. Duru za kitiba na kieneo zimearifu kuwa, wanachama 14 wa vikosi vya kujitolea vya kiraia wakiwemo wapiganaji wa Ansarullah wameuawa katika mapigano na magaidi wa al Qaida katika mji wa Ta'izz wa kusini mwa Yemen. Watu wengine 23 wakiwemo wapiganaji 17 wa Ansarullah wameuawa pia kwenye mapigano na mashambulio ya anga ya Saudia huko katika mji wa Daleh kusini mwa Yemen.
Ndege za kivita za Saudi Arabia leo zimezishambulia wilaya za Lawder na Moudiya katika mkoa wa Abyan wa Yemen. Watu wasiopungua 45 waliuawa jana na mamia ya wengine kujeruhiwa hapo jana kufuatia mashambulizi ya anga ya Saudia mkoani Sa'aada kaskazini magharibi mwa

No comments:

Post a Comment