Sunday, 26 April 2015
Magaidi wazidi kutwangana wenyewe nchini Syria
Habari kutoka nchini Syria zinasema kuwa mapigano baina ya
makundi ya kigaidi yamepamba moto nchini humo. Mtandao wa habari wa an
Nashrah wa nchini Lebanon umetangaza kuwa, leo Jumapili, wanamgambo wa
kundi la kigaidi la Daesh wametwangana na makundi mengine kadhaa ya
kigaidi katika mji wa Mari' mkoani Halab, kaskazini mwa Syria. Kwa
mujibu wa mtandao huo makumi ya magaidi wameuawa kwenye mapigano hayo.
Wakati huo huo jeshi la Syria leo limeendeleza operesheni zake za
kukomboa maeneo mbalimbali kutokana mikononi mwa makundi ya kigaidi
yakiwemo maeneo ya Jisrush Shughur huko Idlib, kaskazini magharibi mwa
Syria na kufanikiwa kuyasafisha kikamilifu maeneo hayo kutoka mikononi
mwa magaidi wanaoungwa mkono na madola ya kigeni na ya kibeberu kama
vile utawala wa Kizayuni wa Israel. Habari nyingine kutoka Syria
zinasema kuwa, leo Jumapili, kundi la kigaidi la Jabhatun Nusra limewaua
kwa umati wananchi 30 wa Syria katika eneo la Jisrush Shughur huko
Idlib, ikiwa ni kuendeleza jinai zake za kila leo dhidi ya wananchi wa
Syria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment