Idadi ya watu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi nchini
Nepal imeongeza na kufikia 3800, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo. Wizara hiyo imetangaza kuwa,
zaidi ya watu 7000 wamejeruhiwa na wengi wao wako katika hali mahututi.
Rameshwor Dangal, mkuu wa Idara ya Kupambana na Majanga iliyo chini ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nepal, amethibitisha habari hiyo na kuongeza
kuwa, watu wengine 90 kati ya wahanga hao, walipoteza maisha nchi
jirani hususan, China na India ambazo nazo zilikumbwa na mtetemeko huo.
Tetemeko la ardhi lililotokea juzi nchini Nepal lilikuwa na ukubwa wa
7,8 kwa kipimo cha rishta, na halijawahi kushuhudiwa nchini humo kwa
kipindi cha miongo minane iliyopita. Tetemeko hilo lilisababisha pia
kuporomoka theluji ya mlima Everest na kuua watu wanamichezo 18 wa skii.
Tayari
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za
rambirambi kwa Rais wa Nepal, Ram Baran Yadav kutokana na maafa hayo
No comments:
Post a Comment