Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Thursday, 23 April 2015

Wamarekani waandamana Baltimore wakidai haki

Wakazi wa mji wa Baltimore nchini Marekani wamefanya maandamano wakitaka kutendewa haki na uadilifu Mmarekani mweusi aliyefariki dunia baada ya kujeruhiwa akiwa mikononi mwa polisi.
Waandamanaji hao walibeba mabango yenye maandishi: "Maisha ya Watu Weusi Yana Thamani". Vilevile wametaka kukomeshwa ubaguzi dhidi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika unaofanywa na vyombo vya dola. Waandamanaji hao pia wametaka kutendewa haki Mmarekani mweusi, Freddie Gray, ambaye amefariki dunia Jumapili iliyopita akiwa hospitalini baada ya kujeruhiwa na polisi ya Marekani. Uchunguzi wa maiti ya mhanga huyo umebaini kuwa Freddie Gray alifariki dunia kutokana na majeraha makali kwenye uti wa mgongo. Mwanasheria wa familia ya Gray anasema kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 25 alipoteza fahamu na baadaye kufariki dunia baada ya kuvunjwa uti wa mgongo akiwa katika korokoro ya Polisi ya Marekani

No comments:

Post a Comment