Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wa
Iran, serikali ya Marekani ndiye inayopasa kutekeleza makubaliano ya
nyuklia na kwamba hitilafu za ndani za nchi hiyo haziizuii nchi hiyo
kutotekeleza ahadi na makubaliano yake ya kimataifa. Muhammad Javad
Zarif amesema kuhusiana na baadhi ya makelele yaliyozushwa ndani ya
Congresi ya Marekani na mivutano kati ya vyama viwili vya nchi hiyo
kuhusu makubaliano ya nyuklia na Iran na kueleza kuwa: Iran inaitambua
serikali ya Marekani kuwa ndiyo inayopasa kutekeleza makubaliano na
kwamba matatizo na mivutano ya ndani ya Marekani haiihusu Iran wala
suala la utekelezaji wa makubaliano hayo. Amesema kwa mujibu wa sheria
za kimataifa, matatizo ya ndani ya nchi, hayatoi kisingizio kwa nchi
hizo kutotekeleza makubaliano yake ya kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo jana alasiri kwa wakati wa New York Marekani.
Muhammad Javad Zarif amelitaja lengo kuu la safari yake huko New York
kuwa ni kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa kuangalia upya mkataba
wa NPT
No comments:
Post a Comment