Sunday, 26 April 2015
Onyo la Naibu Waziri Mambo/Nje wa Iran kwa Saudia
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya
Kiarabu na Kiafrika ameilaumu Saudi Arabia kwa kuzuia misaada ya
kibinadamu ya Iran isiwafikie wananchi wa Yemen. Hussein Amir
Abdollahiyan amesema hayo leo na kuongeza kuwa, vitendo vya Saudia vya
kuizingira Yemen na kuzuia misaada ya kibinadamu ya Iran kuwafikia
wananchi wa nchi hiyo havitaachwa vipite vivi hivi. Ameongeza kuwa,
daima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikihimiza kutumiwa njia za
mazungumzo na kidiplomasia kutatua masuala mbalimbali hata hivyo
ametahadharisha kuwa, Iran inazingatia machaguo yote kwa ajili ya
kuwasaidia wananchi wa Yemen, kuwatumia misaada ya haraka ya kibinadamu
na kuchukua majeruhi wa nchi hiyo kwa ajili ya kuwatibu. Vile vile
amesema kuwa, Saudia haina haki ya kuwapangia cha kufanya watu wengine
na kuonya kuwa, uingiliaji wa kijeshi wa Saudia nchini Yemen ambao
umeshapelekea mamia ya watu kuuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa
sambamba na kuharibiwa miundombinu ya nchi hiyo ya Kiarabu, utapelekea
kuwa mkubwa zaidi mgogoro wa Yemen kwa madhara ya eneo hili zima kwani
hadi hivi sasa matokeo ya uvamizi huo si kitu kingine ghairi ya ukosefu
wa amani ndani ya Saudia kwenyewe na katika eneo hili lote kiujumla
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment