Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Wednesday, 8 April 2015

UN: Jinai za Israel dhidi ya Wapalestina zimezidi

Umoja wa Mataifa umetoa ripoti kuhusu kuongeza jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina. Ripoti ya kila wiki ya Taasisi ya Kimataifa ya Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa huko Palestina imeonyesha kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wiki iliyopita walizishambulia mara 110 nyumba za raia wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwateka nyara Wapalestina 132. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, katika muda wa wiki hiyo moja Wapalestina 64 wakiwemo watoto 5 walijeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kijana wa Kipalestina aliyejeruhiwa  wiki iliyopita na wanajeshi wa Kizayuni ameaga dunia. Katika kipindi hicho cha wiki moja iliyopita, nyumba tatu mali za Wapalestina zilibomolewa pia na wanajeshi wa Israel  katika kijiji kimoja karibu na mji wa Jenin.
Ofisi ya Uratibu wa Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa vile vile imetangaza kuwa kivuko cha Rafah ambacho ni njia pekee inayotegemewa na raia wa Palestina wa Ukanda wa Ghaza ili kuwasiliana na ulimwengu wa nje, kilitaka pia kufungwa wakati fulani

No comments:

Post a Comment