Kongamano la tatu la kimataifa la watafiti na wasomi wakubwa wa
Qur'ani Tukufu limeendelea leo kwa siku yake ya pili huko mjini Fez,
Morocco. Kongamano hilo lililoanza jana na ambalo linajadili kadhia ya
uandishi wa elimu ya misingi ya tafsiri, matukio na malengo,
linahudhuriwa na idadi kubwa ya maulamaa, watafiti wakubwa wa elimu ya
Qur'ani na wataalamu wa nadharia wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu katika fani
ya Tafsiri ya Qur'ani, kutoka Morocco na nchi nyengine za Kiislamu.
Aidha kongamano hilo la siku tatu, mbali na kujadili kadhia ya uandishi
wa misingi ya tafsiri, litajadili pia masuala kwa ujumla ya uandishi wa
elimu ya tafsiri, ikiwemo msingi wa kutegemea vyanzo vikuu ambavyo, ni
Qur'ani na hadithi sahihi za Mtume, maana na lugha ya tafsiri ya
Qur'ani, mambo ambayo yanapewa kipaumbele zaidi na watafiti wa kielimu
kwa ajili ya kutoa mwanya wa kufanyika uchunguzi zaidi wa kitabu hicho
cha Allah. Kando na kongamano hilo, kunafanyika pia maonyesho mbalimbali
ya Qur'ani kwa kuwajumuisha magwiji na weledi wa masuala ya kidini na
pia maonyesho ya vitabu mbalimbali vya
No comments:
Post a Comment