Wanachuo wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Maryland nchini
Marekani wamepongeza na kukaribisha hatua ya kufutwa uamuzi wa kuoneshwa
filamu ya American Sniper.
Wanafunzi hao wamesema hiyo ni hatua nzuri ya kujenga
mazingira ya amani na ya kiadilifu katika chuo hicho. Uamuzi huo
ulichukuliwa baada ya malalamiko ya wanafunzi Waislamu wa Chuo Kikuu cha
Maryland. Wanafunzi hao wanasisitiza kuwa filamu hiyo inavunjia heshima
Uislamu na Waislamu na kueneza hisia za kuhujumu na kupiga vita
Uislamu. Taarifa iliyotolea na jumuiya ya Wanafunzi Waislamu wa Chuo
Kikuu cha Maryland imesema: Filamu hiyo inawadhihirisha Waislamu kuwa ni
hawana utu au kwamba ni watu wasiostaarabika na kueneza fikra ya mauaji
ya umati. Imesisitzia kuwa filamu ya ya American Sniper inawavunjia
heshima na kuwadunisha Waislamu kote duniani.
Waislamu katika vyuo vikuu vingine vya Marekani pia
wametaka kusimamishwa zoezi la kuoneshwa filamu hiyo na wamekuwa
wakitumia nyenzo mbalimbali kueleza malalamiko yao.
Filamu iliyotengenezwa Marekani ya American Sniper inaeleza
kisa cha Chris Kyle askari wa Marekani aliyetumwa mara kadhaa kupigana
nchini Iraq. Kyle ambaye aliuawa mwaka 2013 alikuwa mwanachama wa Jeshi
la Majini la Marekani ambaye anashikilia rekodi ya kuua watu 160 kati
ya walenga shabaha wa Kimarekani
No comments:
Post a Comment