Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali mauaji ya
kinyama yaliyofanywa na kundi la kigaidi la Daesh dhidi ya Wakristo 30
wa Ethiopia ambao waliuawa kinyama kwa kuchinjwa huko Libya. Taarifa ya
wanachama 15 wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imelaani vikali
mauaji hayo na kubainisha kwamba, kitendo hicho cha Daesh kimethibitisha
kwa mara nyingine tabia ya unyama na ukatili liliyo nayo kundi hilo.
Baraza la Usalama limesisitiza kuwa, jinai za Daesh hazina mpaka na
kwamba, kundi hilo limekuwa likitenda jinai na mauaji bila ya kujali
thamani za kiutu na kibinadamu; na hivyo kuwa adui wa mataifa yote.
Taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa, kuna
haja ya kuchukuliwa hatua kali za kukabiliana na kundi hilo ambalo
limekuwa likifanya mauaji ya kutisha. Kundi la kigaidi na kitakfiri la
Daesh hivi karibuni lilitoa mkanda wa video unaoonyesha wanachama wa
kundi hilo wakiwachinja Wakristo wasiopungua 30 raia wa Ethiopia nchini
Libya. Mkanda huo wa video wa dakika 29 unaonyesha magaidi wa Daesh
wakiwauwa kwa kuwachinja Wakristo 16 wa Ethiopia katika pwani moja huko
Libya na kuwaua wengine kwa kuwapiga risasi katika eneo la jangwani.
No comments:
Post a Comment