Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Thursday, 23 April 2015

Jeshi la Nigeria ladhibiti ngome ya Boko Haram

Jeshi la Nigeria limefanikiwa kukomboa msitu wa Sambisa ambao ulikuwa ngome ya mwisho inayotambulika ya kundi la kigaidi la Boko Haram.
Taarifa iliyotolewa jana na maafisa wa jeshi la Nigeria imesema, operesheni hiyo inafanyika kwa ajili ya kukomesha uasi wa miaka 6 wa kundi la Boko Haram nchini humo. Majeshi ya nchi za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon yanashirikiana kwa miezi miwili sasa kwa ajili ya kuliangamiza kundi hilo la kigaidi.
Msitu wa Sambisa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria uko umbali wa karibu kilomita 100 kutoka kijiji cha Chibok ambako mwaka mmoja uliopita kundi la Boko Haram liliteka nyara zaidi ya wasichana 200 wa shule na kuwapeleka kusikojulikana. Kutekwa nyara kwa wasichana hao wanafunzi kulielekeza macho ya jamii ya kimataifa kwa mgogoro mkubwa wa kibinadamu uliosababishwa na mashambulizi ya kundi hilo la kigaidi nchini Nigeria

No comments:

Post a Comment