Timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran jana jioni ilikamilisha
duru mbili za mazungumzo na Naibu Mkuu wa Siasa za Nje za Umoja wa Ulaya
mwanzoni mwa mashauriano ya jinsi ya kuandika matini ya makubaliano ya
mwisho ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1.
Mazungumzo hayo yaliyoikutanisha timu ya nyuklia ya Iran na Helga-Schmid, yamehudhuriwa pia na wataalamu wa pande hizo mbili.
Timu ya nyuklia ya Iran mapema leo itakutana na kufanya mazungumzo na kiongozi wa timu ya Marekani katika mazungumzo ya nyuklia, Wendy Sherman. Manaibu Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika kundi la 5+1 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani pia watajiunga na mazungumzo ya nyuklia ya Iran Ijumaa ya kesho.
Jana Jumatano lilianza rasmi zoezi la kuandika matini na makubaliano ya mwisho ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 mjini Vienna, Austria

No comments:
Post a Comment