Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amekaribisha ripoti ya Umoja
wa Mataifa iliyoshutumu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel
katika shule ya umoja huo katika eneo la Ukanda wa Ghaza.
Waziri wa mambo ya Nje wa Palestina Riyadh al Maliki Jumanne hii
amekaribisha ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyolaani mashambulizi ya
Israel dhidi ya shule inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa huko Ukanda
Ghaza wakati wa mashambulizi ya siku 50 yaliyoanzishwa na Israel katika
msimu wa joto mwaka uliopita na kusema kuwa, kopi ya ripoti hiyo
itawasilishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa ajili ya
uchunguzi.
Riyadh al Maliki ameongeza kuwa, ripoti ya Umoja wa Mataifa
iliyoshutumu mashambulizi ya mwaka jana ya utawala wa Kizayuni wa Israel
katika shule ya UN huko Ghaza, inahusiana na uchunguzi wa awali ambao
tayari umeanza katika mahakama ya ICC na kwamba ripoti hiyo itasaidia
sana kupata matokeo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina amesisitiza
ulazima wa kufanywa uchunguzi rasmi kuhusu mashambulizi ya utawala wa
Kizayuni wa Israel huko Ghaza na mauaji yaliyofanywa na utawala huo
mtenda jinai dhidi ya raia wa Palestina wasio na hatia wa eneo hilo.
Maelfu ya wapealestina waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi hayo ya Israel
No comments:
Post a Comment