Polisi ya Burundi leo imemkamata kinara wa wanaharakati wa
kutetea haki za bininadamu nchiniu humo, Pierre-Claver Mbonimpa,
kufuatia machafuko na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga
uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa kogombea kiti cha rais kwa mara ya
tatu.
Vilevile vyombo vya usalama vya Burundi vimetoa waranti wa
kutiwa nguvuni Vital Nshimirimana ambaye ndiye anayeongoza kampeni ya
kumzuia Mkurunzinza asiwania tena urais kwa awamu ya tatu.
Wakili wa
Mbonimpa, Armel Niyongere, amesema mteja wake hakuelezwa tuhuma
zinazomkabili na kwamba anaamini amekamatwa kutokana na kuwataka
wananchi washiriki kwenye maandamano ya leo. Walioshuhudia wamesema
polisi walimpiga makofi na mateke mwanaharakati huyo.
Ghasia na
machafuko yameendelea leo nchini Burundi huku wananchi wakiandamana
kupinga uamuzi wa chama tawala cha CNDD-FDD wa kumuidhinisha Mkurunziza
kuwania tena kiti cha rais. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Msalaba
Mwekundu nchini Burundi Alexis Manirakiza amesema watu 6 waliuawa katika
machafuko ya jana mjini Bujumbura.
No comments:
Post a Comment