Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Tuesday, 21 April 2015

Maandamano ya wapinzani yaongezeka nchini Guinea

Maandamano ya kuipinga serikali ya Guinea yameanza upya na kwa kasi kubwa, kufuatia machafuko mabaya yaliyotokea wiki iliyopita kati ya polisi na waandamanaji.
Maandamano hayo yamefanyika katika miji mbalimbali ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika vikiwemo pia viunga vya mji mkuu, Conakry.
Katika maandamano ya jana, waandamanaji walichoma moto matairi ya gari wakafunga njia na kutoa nara za kuipinga serikali.
Mamlaka husika ziliweka ulinzi mkali katika maeneo mengi ya Caonakry ili kuzuia kutokea mambo yasiyotakiwa.
Hata hivyo polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji baada ya waandamanaji hao kuwalenga kwa mawe polisi.
Serikali ya Guinea imetoa tamko na kusema kuwa maandamano ya namna hiyo yanalisababishia hasara kubwa taifa hilo

No comments:

Post a Comment