Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Friday, 10 April 2015

Mkapa: Vita vya tatu vya dunia vinaweza kutokea

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa amezitaka nchi za Kiafrika kukuza uongozi bora na kuachana na mikataba mibovu isiyojali ustawi wa wananchi kwa kuwa inaweza kuzipeleka katika vita. Miongoni mwa mikataba ambayo  Mkapa amesema kuwa ni mibovu na isiyofaa, hivyo iepukwe ni wa Kiuchumi baina ya Mataifa ya Afrika, Caribbean na Pacific ili kuepusha vita, ambavyo kwa sasa vitakuwa ni vya kiuchumi. Aidha, Rais huyo mstaafu ametaka muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ufanyiwe marekebisho ili kuongeza nchi nyingine ambazo zinastahili kuingia kwa sasa. Benjamin Mkapa amesisitiza kuwa, kwa hali ilivyo sasa ni sababu za kiuchumi ndizo zinazoleta vita, kutokana na uongozi mbaya, njaa na kiu ya baadhi ya nchi kutaka maliasili za mataifa mengine. Mkapa amesema kama ninavyomnukuu: “Hatutarajii kuwa na vita kama ile ya pili ya dunia, kwa sababu dunia sasa inamiliki silaha kali kama za nyuklia, zinazoweza kuangamiza maisha kwa wingi. Amesema ili kuzuia vita kutokea ndani ya nchi, ama kati ya nchi mbili, ukanda, bara na hata dunia, kuna umuhimu wa serikali zilizoko madarakani na hasa barani Afrika kuwekeza kwenye uongozi bora na kuwashirikisha wananchi katika maamuzi ya kidemokrasia, yanayohusu maisha na rasilimali za nchi zao

No comments:

Post a Comment