Rais Hassan Rouhani amesema kulinda
maisha na usalama wa watu, kutetea izza ya Ulimwengu wa Kiislamu na Umma
wa Kiislamu na kuleta ustawi ni majukumu matatu muhimu waliyonayo
Waislamu wote duniani. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito
huo jioni ya leo mjini Jakarta, Indonesia mbele ya hadhara ya maulama,
wakuu, wasomi na shakhsia wa vyuo vikuu vya nchi hiyo na kusisitiza
kwamba Waislamu wote wanapaswa kuvunja kimya chao mbele ya makundi ya
kigaidi ambayo yameuhasiri vibaya zaidi Uislamu na kupaza sauti zao kwa
pamoja kukabiliana na vitendo vya ukatili, kufurutu mipaka na ugaidi.
Huku akisisitiza kuwa kuleta umoja katika Ulimwengu wa Kiislamu ndilo
jukumu muhimu zaidi la Waislamu, Hujjatul Islam Rouhani amesema Uislamu
ni dini ya wastani, mantiki na busara, na kwamba jukumu la Waislamu wote
ni kuwabainishia walimwengu Uislamu halisi. Amesema leo hii kuna baadhi
ya watu katika Ulimwengu wa Kiislamu ambao wameichafua izza ya Uislamu;
na kwa kutumia jina la jihadi na dini wameinua panga kumuelekezea Mtume
Mtukufu SAW; hivyo Waislamu wote wanapaswa wajihisi kuwa na jukumu la
kukabiliana na hali hiyo. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
amebainisha kuwa Uislamu umeenea ulimwenguni kutokana na wito wake wa
mantiki na upendo na kusisitiza kwamba Uislamu si dini ya upanga, bali
ni dini ya mantiki, urehemevu, upendo na kuishi kwa amani na watu
wengine na katu haumlazimishi mtu yeyote kuufuata…/
No comments:
Post a Comment