Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, sababu ya kushuhudiwa wimbi hilo kubwa la wakimbizi ni mapigano makali yanayoendelea kati ya jeshi la Iraq na makundi ya kigaidi na kitakfiri katika mkoa wa al Anbar wa magharibi mwa nchi hiyo.
Hatua kali za kiusalama zimechukuliwa mjini Baghdad kutokana na kuingia idadi hiyo kubwa ya wakimbizi.
Shirika la Hilali Nyekundu la Iraq limeanza kuchukua hatua za kuwahifadhi wakimbizi hao kwa kushirikiana na serikali.
Kwa upande wake, Lise Grande, mratibu wa masuala ya misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amesema leo kuwa, wakimbizi kutoka mkoa wa al Anbar wanahitajia mno misaada ya kibinadamu.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mtu anaumia moyoni anapowaona watu wakikimbia kwa kasi kubwa na kama waliochanganyikiwa kutafuta sehemu salama ya kuishi
No comments:
Post a Comment