Unordered List


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Tuesday, 28 April 2015

Ban apinga utumiaji wa nguvu za jeshi dhidi ya wahajiri


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepinga hatua yoyote ya kutumia nguvu za jeshi katika suala na wahajiri haramu wanaoelekea Ulaya kupitia Libya na Bahari ya Mediterranean.
Ban Ki-moon amesema utumiaji wa mabavu hauwezi kutatua mgogoro wa maafa ya wahamiaji haramu katika Bahari ya Mediterranean. Amesema kuna udharura wa kuanzishwa mpango kamili na wa kisheria kwa ajili ya wahajiri hao kwa kutilia maanani usalama na haki za wahajiri.
Mwishoni mwa kikao chake cha Alkhamisi iliyopita kilichojadili suala la kughariki wahajiri 900 katika Bahari ya Mediterranean, Umoja wa Ulaya umeazimia kuchukua hatua kali za kuzuia maafa hayo ikiwa ni pamoja na kuzisaka boti na meli zinazowapakia na kuziharibu. Vilevile kulizungumziwa suala la kutumia nguvu za jeshi kukabiliana na magenge yanayotorosha watu kuelekea Ulaya kupitia bahari hiyo.

No comments:

Post a Comment