Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh limetoa mkanda wa video
unaonyesha kundi hilo likiwachinja Wakristo wasiopungua 30 raia wa
Ethiopia ambao walitekwa nyara na kundi hilo huko Libya. Mkanda huo wa
video wa dakika 29 uliotolewa leo na kundi la kigaidi la Daesh
unaonyesha magaidi wa Daesh wakiwauwa kwa kuwachinja raia wa Ethiopia wa
dini ya Kikristo wasiopungua 12 katika pwani moja huko Libya na pia
likiwapiga risasi kundi jingine la mateka 16 katika eneo la jangwani.
Idadi kamili ya wahanga wa ukatili huo wa Daesh bado haijafahamika.
Kundi la kigaidi la Daesh limeshaonyesha mikanda kadhaa ya video za
ukatili na mauaji liliyoyafanya dhidi ya watu liliowateka nyara raia wa
nchi mbalimbali kama Iraq, Syria, Marekani, Uingereza na Japan. Tarehe
15 mwezi huu mbunge mmoja wa Iraq ajulikanae kwa jina la Adel Khamis al
Mahlawi alisema katika mkutano na vyombo vya habari kuwa, magaidi wa
Daesh wamewauwa kwa kuwakata vichwa watu wasiopungua 300, ambao wengi
wao wanaaminika ni kutoka makabila ya wanaohamahama katika mkoa wa al
Anbar magharibi mwa Iraq
No comments:
Post a Comment