Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka yaanzishwe
mara moja mazungumzo ya kuleta amani nchini Yemen. Akihutubia kwenye
mkutano wa kimataifa wa kukabiliana na jinai unaofanyika Doha, mji mkuu
wa Qatar Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza juu ya kukomeshwa
haraka mashambulizi ya kijeshi ya Saudi Arabia nchini Yemen sanjari na
kuanzishwa mchakato wa mazungumzo ya kutafuta amani nchini humo. Ban Ki
moon ameiambia Saudi Arabia na waitifaki wake kwenye machafuko ya Yemen
kwamba, Umoja wa Mataifa uko tayari kuanzisha mchakato wa mazungumzo ya
kutafuta amani nchini humo. Ban Ki moon amesisitiza kuwa, mazungumzo ya
amani pekee ndiyo yatakayoweza kuutatua mgogoro wa Yemen. Takwimu
zinaonyesha kuwa, wahanga wakuu wa mashambulio ya kijeshi ya Saudi
Arabia na waitifaki wake nchini humo ni wanawake na watoto.
No comments:
Post a Comment