Monday, 27 April 2015
Al Marzouq: Malengo ya mapinduzi Tunisia hayajafikiwa
Rais wa zamani wa Tunisia amesema kuwa malengo ya Mapinduzi ya
Januari 14 2011 hayajafikiwa nchini humo.Monsif al Marzouq Rais wa
zamani wa Tunisia amesema kuwa tunapasa kukiri kuwa malengo na matakwa
ya wananchi wa Tunisia kutokana na Mapinduzi ya mwezi Januari mwaka 2011
hayajafikiwa, kutokana na mapinduzi yaliyojiri dhidi ya mapambano hayo
ya ukombozi. Al Marzouq ameashiria hali ya kiuchumi isiyoridhisha ya
Tunisia kutokana na uchumi wa nchi kuwa tegemezi na kueleza kuwa,
Tunisia imeshindwa kuboresha misingi ya kidemokrasia ya amani nchini na
hadi sasa haijaweza kukomesha machafuko katika jamii kwa kuwaandalia
wananchi mazingira mazuri na salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment